Sunday, January 11, 2015

UJENZI WA DARAJA

Picha hizi zinaonesha tukiwa site kwenye ujenzi wa daraja mkoani Tanga, mwezi December 2014.

Friday, January 9, 2015

JINSI YA KUCHAGUA SAKAFU NZURI KWA AJILI YA NYUMBA YAKO


Siku hizi kutokana na mapinduzi ya kiteknolojia nyumba zetu husakafiwa kwa unadhifu wa hali ya juu kwa kutumia Tiles ama mbao kusakafia hata wale wanaosakafia kwa cement basi huzipaka rangi na kuvutia na kutoa mng'aro wa aina yake ambao hufanya nyumba kuonekana safi na yenye mvuto. 

VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUSAKAFIA

  1.  Rangi - Chagua rangi itakayolandana vyema na samani zako za ndani ikiwa ni pamoja na rangi ya nyumba yako. Kumbuka rangi ang'avu kama nyeupe hupendeza sana ila huchafuka haraka na usafishaji wake hasa kwenye tiles si rahisi ukilinganisha na rangi nyingine hafifu kama nyeusi, kijivu au brown na ndio maana nyumba nyingi huku kwetu kulingana na vumbi husakafiwa na tiles/marumaru zenye rangi hafifu. 
  2. Ubora na uimara - chagua sakafu bora na imara kulingana na shughuli za sehemu husika. Ikiwa ni eneo linalotumika sana au lenye kupishwa vitu vizito jitahidi kuweka sakafu itakayokidhi na kustahmili shughuli za eneo husika. 
  3. Comfort - Chagua sakafu ambayo haitawakwaza baadhi ya watu kulingana na umri wao yaani iwe salama kwa watoto, wazee, wagonjwa na vijana. Kwa maeneo yenye unyevu kama utachagua kuweka tiles basi hakikisha hazitelezi kiasi cha kufanya watu kuanguka haswa bafuni. Mara nyingi hua tunafanya kosa la kuweka tiles za kuteleza mpaka bafuni hali inayosababisha watu kuanguka ilihali ni hatari na ukiweza kuepuka basi fanya hivyo. 
  4. Gharama - Chagua sakafu kulingana na budget yako pamoja na shughuli za eneo husika.

Thursday, January 8, 2015

VITU VYA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA KIWANJA

Je ni kwajili ya shughuli za kilimo, nyumba ya kuishi au biashara, kiwanda nakadhalika. Kumbuka kuwa nyumba au ardhi ni hazina kubwa hivyo hakikisha na ni sehemu sahihi ya shughuli yako. Kama ni eneo la kamazi na unataka kujenga nyumba ya kuishi basi zingatia haya:- 
  • Hakikisha muuzaji anatoa hati sahihi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi uliyoko. 
  • Hakikisha ni eneo salama na linalofikika, hapaathiriwi na mafuriko, wala mmomonyoko wa udongo. 
  • Pia pasiwe ni karibu na viwanda hatarishi kwa malezi ya watoto Pawe karibu na huduma muhimu kama soko, msikiti au kanisa, shule, stendi ya mabasi, hospitali na huduma nyingine muhimu . 
  • Ni vema pia kuangalia Udongo wa eneo husika kama ni sahihi kwa aina ya shughuli unayotaka kufanya au nyumba unayotaka kujenga. 
  • Ni vizuri pia kujua kama ni eneo ambalo limepimwa kwa ajili ya makazi ili kuepuka kuvunjiwa yako. 
  • Je, panamvuto au mwonekano unaotaka wewe? Je kipo ndani ya bajeti yako? Vipi hali ya upatikanaji wa maji na umeme katika eneo hilo? 
Ukijiridhisha vya kutosha kulingana na matakwa yako ndipo uamue kununua au kuacha.