Siku hizi kutokana na mapinduzi ya kiteknolojia nyumba zetu husakafiwa kwa unadhifu wa hali ya juu kwa kutumia Tiles ama mbao kusakafia hata wale wanaosakafia kwa cement basi huzipaka rangi na kuvutia na kutoa mng'aro wa aina yake ambao hufanya nyumba kuonekana safi na yenye mvuto.
VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUSAKAFIA
- Rangi - Chagua rangi itakayolandana vyema na samani zako za ndani ikiwa ni pamoja na rangi ya nyumba yako. Kumbuka rangi ang'avu kama nyeupe hupendeza sana ila huchafuka haraka na usafishaji wake hasa kwenye tiles si rahisi ukilinganisha na rangi nyingine hafifu kama nyeusi, kijivu au brown na ndio maana nyumba nyingi huku kwetu kulingana na vumbi husakafiwa na tiles/marumaru zenye rangi hafifu.
- Ubora na uimara - chagua sakafu bora na imara kulingana na shughuli za sehemu husika. Ikiwa ni eneo linalotumika sana au lenye kupishwa vitu vizito jitahidi kuweka sakafu itakayokidhi na kustahmili shughuli za eneo husika.
- Comfort - Chagua sakafu ambayo haitawakwaza baadhi ya watu kulingana na umri wao yaani iwe salama kwa watoto, wazee, wagonjwa na vijana. Kwa maeneo yenye unyevu kama utachagua kuweka tiles basi hakikisha hazitelezi kiasi cha kufanya watu kuanguka haswa bafuni. Mara nyingi hua tunafanya kosa la kuweka tiles za kuteleza mpaka bafuni hali inayosababisha watu kuanguka ilihali ni hatari na ukiweza kuepuka basi fanya hivyo.
- Gharama - Chagua sakafu kulingana na budget yako pamoja na shughuli za eneo husika.
No comments:
Post a Comment